Back to top

Sheria inayopiga marufuku uzao wa mbwa aina nne walalamikiwa uingereza

17 October 2018
Share

Sheria ya Uingereza inayopiga marufuku ya uzao wa mbwa wa aina fulani ikiwemo Pit Bull terrier,Japanese Tosa,Dogo Argentino na Fila Brasileiro imelalamikiwa na baadhi ya raia wa nchi hiyo wakidai kuwa inakiuka misingi ya haki za wanyama ikiwemo mbwa. 

Uzao wa mbwa hao umetanagzwa kuwa ni hatari kwa wananchi iwapo wataachwa huru kupita mitaani huku sheria hiyo ikiienda mbali zaidi na kuwataka wamiliki wa uzao wa mbwa hao kuhakikisha wanawafunga kifaa maalum katika midomo yao wanaposafirishwa kutoka eneo moja kwenda jingine ila kuwahakikishia wananchi usalama wao 

Hata hivyo kamati ya bunge ya masuala ya mazingira, chakula na masuala ya kijamii nchini humo imeomba kupitiwa upya kwa sheria hiyo.