
Maaskofu na waumini wa madhehebu ya kikristo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa wamelaani tabia za baadhi ya viongozi wa kidini kujihusisha na biashara haramu ya binadamu ambapo wameomba serikali kupitia upya na kuifanyia marekebisho sheria inayoruhusu uanzishwaji wa makanisa ambayo yamekuwa yakikiuka misingi na sheria za nchi.
