Back to top

Shida ya maji, wananchi wafukuzana na Chui Mtwara.

07 October 2021
Share

Wananachi wa kijiji cha Mdui kata ya Mbawala wilaya Mtwara wamesema wanalazimika kufukuzana na wanyama wakali porini akiwemo chui kwa ajili ya kujipatia maji ambayo si safi na salama.

Wakizungumza ITV iliyotembelea kijiji hicho baadhi ya wananchi wamesema wanalazimika kusaka maji katika mabonde yaliyoko maporini kutokana na miundombinu ya maji iliyopo kijijini hapo kutokuwa na maji ya uhakika na hivyo kuatarisha maisha yao.

Kufuatia hilo wameiomba serikali kushughulikia changamoto hiyo ambayo imekuwa ikipelekea kuishi kwa hofu kutokana na kufukuzana na wanyama wakali porini akiwemo chui ili kupata maji kwa ajili ya matumizi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (NTUWASA) Mhandisi Festo Fulgensi amesema miundo mbinu chakavu inachangia kijiji cha Mdui kutopata maji ya uhakika.

Hata hivyo amesema taarifa hizo tayari zimefika Wizara ya Maji na Mwishoni mwa mwezi huu fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu  ya maji kwa mkoa wa Mtwara ikiwemo kijiji cha mdui zitawasili na kuwaomba wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ambacho serikali inashughulikia kero hiyo.