Back to top

SHIDA YA MAJI YAONGEZA GHARAMA ZA UJENZI TANDAIMBA.

23 November 2021
Share

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Tandaimba mkoani Mtwara kimesema ujenzi wa vyumba vya madarasa 88 yanayogharimu shilingi Bilioni 1.6 unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji yanayochangia ongezeko la gharama katika ujenzi.
.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandaimba Baisa Abdallah amesema licha kuwapo kwa mchanga na saruji maji ni tatizo.
.
Amesema ili kuendana na muda uliyopangwa katika kukamilisha madarasa themanini na nane ya fedha zilizotokana na Covid-19 maeneo yaliyopata mradi huo wanalazimika kununua maji maeneo yanapopatikana ili miradi hiyo iweze kumalizika kwa muda uliyopangwa.
.
Amesema kutokana na hilo wanaimani gharama za ujenzi wa madarasa hayo zitaongezeka hivyo amewataka watendaji kutojali gharama hiyo na badala yake kufanya kazi usiku na mchana ili madarasa hayo yakamilike.
.
Kupande wao baadhi ya madiwani wamesema wanapata wakati mgumu katika ujenzi wa marasa hayo na kuiomba serikali kuu kukarabati  miundombinu ya maji ambayo ni chakavu na uwezo wake ni mdogo kufikisha maji kwa wananchi wa wilaya ya Tandaimba.