Back to top

Shughuli za uchimbaji mdogo kuendelea katika mgodi wa Shilalo.

18 October 2019
Share

Serikali imeruhusu tena kuendelela kwa shughuli za uchimbaji mdogo wa madini katika mgodi wa Shilalo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, baada ya Mkuu wa mkoa wa  Mwanza kusitisha uchimbaji kwenye maduara 38 kati ya 57 yaliyopo kwenye mgodi huo Oktoba 7 mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Waziri wa Madini Dotto Biteko baada ya kukutana na wachimbaji wadogo wa mgodi huo ikiwa ni baada ya siku 10 tangu Mkuu wa mkoa huo John Mongella alipositisha shughuli za uchimbaji.