Back to top

Shule ya msingi Burungura yakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

20 July 2021
Share

Shule ya msingi BURUNGURA yenye wanafunzi zaidi ya mia nane iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na ukosefu wa walimu wa kike hali inayosababisha utoro kwa wanafunzi wa kike kwa kushindwa kuhudhuria masomo yao wakati wa hedhi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa wilaya hiyo kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi pamoja na kuhamasisha miradi ya maendeleo, baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wamesema kuwa ukosefu wa walimu wa kike umekua chanzo kikubwa cha utoro shuleni hapo.

Mkuu wa wilaya ya Muleba Toba Nguvila amemtaka Afisa Elimu wa Shule za msingi wilayani humo kufanya uhamisho wa haraka wa walimu wa kike waliorundikana katika shule za msingi zilizopo mjini muleba ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wa shule ya msingi Burungurakwa lengo la kuinua ufaulu wa wanafunzi hao.

Shule ya msingi BURUNGURA ina wanafunzi mia nane sitini na nane, walimu watano.