Shule ya msingi Mnyonga ambayo ni ya mchanganyiko pamoja wanafunzi wenye Ulemavu iliyoko Peramiho mkoani Ruvuma inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madarasa ambapo kati ya madarasa kumi na mbili yanayotakiwa kwasasa ina madarasa manne tu.
Changamoto hizo zimeelezwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Mwalimu Monica Kasia ambapo amesema kuwa shule hiyo pia ina upungufu wa Madawati wanafunzi wanakaa chini, ukosefu wa Bwalo la kulia hivyo wanafunzi hula wakiwa wameketi kwenye Nyasi na pia haina Jiko na hivyo Mpishi hupika akainyeshewa na mvua.
Kutokana na changamoto hiyo jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Songea vijijini imetoa misaada mbalimbali kupunguza baadhi yachangamoto zinazoikabili shule hiyo.