Back to top

Shule ya msingi yenye walimu wawili Njombe.

25 March 2020
Share

Wananchi wa kijiji cha Nindi kilichopo kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wametoa kilio chao kwa serikali wakiomba wasaidiwe walimu katika shule ya msingi Nindi baada ya walimu wawili waliopo kutajwa hawatoshi na kusababisha adha kwa wanafunzi.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema serikali italifanyia kazi tatizo la uhaba wa walimu mara moja.