Back to top

Shule zote za Kenya kufunguliwa Januari 4 mwaka wa 2021.

16 November 2020
Share

Baada ya  wanafunzi wengi kukaa nyumbani kwa zaidi ya miezi 9, huku watahiniwa pekee wakiwa ndio walioko shuleni, hatimaye Wizara ya Elimu nchini Kenya imetangaza kwamba shughuli zote za masomo kote nchini Kenya zitafunguliwa tarehe 4 mwezi Januari mwaka ujao na muhula wa kwanza kukamilika.


Akitangaza hayo,Waziri wa Elimu Prof. George Magoha amesema kwamba hili limeafikiwa kufuatia mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta ya elimu na kukubaliana kwa pamoja kuhusu tarehe hiyo ikiwemo tarehe za kufanya mitihani.

Haya yanajiri huku idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini ikifikia 70,804 baada ya watu wengine 559 kuambikizwa ndani ya saa 24 zilizopita.