
Kamishina wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Bwana RODGERS SIANG'A amesema kuna kigogo wa uingizaji wa kemikali zisizoruhusiwa nchini anayeishi Mkoani Mwanza alitaka kumuhonga Shilingi Milioni mia- nane ili aharibu ushahidi katika kesi inayomkabili.
Mbali ya hilo Kamishina SIANG'A pia amesema mmoja kati ya makamishina katika ofisi yake ambaye ni mmoja kati ya wasaidizi wake wakuu, aliahidiwa rushwa ya Shilingi Milioni mia- nne ili amuunganishe mfanyabiashara huyo na Kamishina SIANG'A na baadaye waharibu ushahidi kwa pamoja.
Kamishina Siang'a ameiambia Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za Kulevya kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akiingiza kemikali hizo kwa muda mrefu wakati anajua haziruhusiwi na alikuwa akitumia uwezo wake wa fedha katika kuharibu ushahidi kila anapokamatwa na alithubutu kutaka kumuhonga hadi yeye.
Amesema ushahidi wa kitaalam umebaini kuwa kemikali hizo zikichanganywa na nyingine zinaweza kinachopatikana ni dawa za kulevya hivyo mamlaka yake itaendelea kusimamia kikamilifu azma ya kuhakikisha uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya nchini vinakomeshwa.