Back to top

SILAA ATOA SIKU 14 KUKAMILISHA MPANGO WA BANDARI KAVU TUNDUMA

09 June 2024
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumuelekeza Msimamizi wa Mradi wa Kupanga Kupima na Kumilikisha Ardhi afike katika Halmashauri ya mji wa Tunduma mkoani Mbeya ndani ya saa 72 kwa lengo la kuweka mikakati ya ujenzi wa eneo la bandari kavu.

Waziri Silaa amezungumza hayo wakati wa ziara ya kushtukiza alipotembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu ya mjini wa Tunduma akiwa njiani kuelekea mkoani Rukwa.

Aidha, Waziri Silaa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaelekeza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani na Mthamini Mkuu wa Serikali kufika ndani ya siku 9 katika eneo hilo ili kulipanga, kulipima na kutatua changamoto zote za uthamini kwa ajili ya kuharakisha uendelezaji wa mpango huo.