
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, ameahidi kufanya mabadiliko makubwa kwa watumishi wa sekta ya ardhi Jijini Mwanza, baada ya kuwepo kwa vilio vingi vya wananchi waliodhulumiwa ardhi zao ambapo chanzo kikuu kikionekana ni watumishi wa sekta hiyo Jijini Mwanza.
Miongoni mwa wakazi walio na vilio ni Theopista Alphonce kutoka Mtaa wa Nyasaka Jijini humo ambaye anaangua kilio mbele ya watu baada ya kuluwezeshwa na Waziri Silaa kupata haki yake iliyokuwa inamsumbua kwa muda mrefu wakidai.
Waziri Silaa amesema hayo katika viwanja vya Nyamagana ambapo Kliniki ya Ardhi ilikuwa ikifanyika kwa wakazi wa Jiji hilo, kuwasilisha kero zao za ardhi na kutatuliwa papo hapo.
