Back to top

SILAA - "NIMETUMWA KUFIKIA WANANCHI NA KUTATUA MIGOGORO"

28 January 2024
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa, amesema Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amemtuma afike na akutane na wananchi ili kutatua migogoro ya ardhi ndio maana yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta inayotaraji kujadili na kufanya maamuzi ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Vijiji 975 hivi karibuni.

Silaa amesema Kamati hiyo inatarajia kukutana wakati wa Kikao cha Bunge linalotarajiwa kuanza tarehe 30 Januari 2024 na miongoni mwa migogoro inayotarajiwa kutolewa maamuzi ni ule wa wananchi wa Kijiji cha Ruvu kilichopo Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

Waziri Silaa ameyasema hayo Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro katika mkutano na wanakijiji wa Ruvu Darajani ambapo amesema maamuzi yatakayotolewa na kamati hiyo hayatamuumiza mwananchi yeyote kwani ndio maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande Mwingine Waziri Silaa ambaye ndio Mwenyekiti wa Kamati hiyo, amewataka wananchi hao kuendelea na shughuli za kilimo hasa kwa mazao ya muda mfupi pasipo kujiongezea mashamba  au kuvamia mipaka iliyowekwa kwa ajili ya pori tengefu