Back to top

Simba 15 wauawa kwa kutegewa sumu Serengeti na Ruaha

22 June 2018
Share

Jumla ya simba 15 wameuwawa kwa kutegewa sumu kwenye Mbuga ya Serengeti na hifadhi ya taifa ya Ruaha kwa kipindi cha mwezi January hadi June mwaka huu katika matukio ya kulipiza kisasi yanayofanywa na binadamu dhidi ya wanyama ikiwa ni ongezeko la simba 13 ikilinganishwa na mwaka jana 


Akizungumzia matukio hayo muhifadhi mkuu wa mamlaka ya hifadhi za wanyamapori Tanzania TANAPA Christopher Timbuke amesema yanathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za utalii na kuharibu ikolojia ya uhifadhi huku pia serikali ikipoteza mapato yake 

Mratibu wa taifa wa mradi wa uhifadhi na utalii kusini mwa Tanzania Spanest Godwell Ole Meing'ataki anasema ili kudhibiti ongezeko la matukio hayo mamlaka zinazohusika na uhifadhi zishirikishe jamii katika shughuli za uhifadhi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu athari za ujangili na mauaji ya wanyamapori.

Kwa upande wao wadau wa utalii na uhifadhi kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini wanasema wamejiwekea mikakati mbalimbali ya kulinda maliasili katika maeneo hayo  huku wakiiomba serikali kuboresha miundombinu kwenye vivutio vya utalii ili yaweze kufikika kwa urahisi.