Back to top

SINA TAMAA YA MADARAKA NIMERIDHIKA NA NG'OMBE

06 July 2023
Share

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amedai kuwa ameridhika na ufugaji wa ng'ombe wake nyumbani na hana tamaa ya madaraka.
.
Kiongozi huyo ameyasema hayo, wakati akimpigia kampeni Mgombea wa Ubunge wa Oyam Kaskazini, Bw.Samuel Engola, kupitia tiketi ya chama cha National Resistance Movement (NRM), ambaye anawania nafasi hiyo, ili kuchukua nafasi ya Charles Okello Engola aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake Mei 2, 2023.
.
Aidha alisema nia ya chama chake ni kuwatumikia wananchi wa Uganda, na kwamba wataendelea kujitolea kufanyia kazi mageuzi ambayo marehemu Egola aliyaanza.