
Serikali imeingiza zaidi ya Tsh. Bil. 3.5/= kwenye akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha ambayo itatumika kujenga shule ya wasichana ya kimkoa ya mchepuo wa Sayansi itayoanzia kidato cha kwanza hadi cha sita ili watoto wa Mkoa wa Kilimanjaro wapate fursa ya kupata elimu bora ya Sayansi.
.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Siha, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Dkt.Godwin Mollel, wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
