Back to top

SMZ yaahidi utatuzi ajira kwa vijana.

26 June 2022
Share

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutatua changamoto ya ajira hususan kwa vijana kwa kuwawezesha katika maeneo mbalimbali ikiwemo mafunzo pamoja na vifaa vitavyowasaidia katika shughuli wanazozifanya.

Katibu Mkuu Kazi na Uwezeshaji Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Bi Khadija Khamis Rajab ameyasema hayo  wakati wa kufungua kikao cha kamati ya kuratibu masuala ya ajira kwa vijana kupitia kamati za Zanzibar katika ukumbi wa Hospitali ya wagonjwa wa akili Kigongo Chekundu wilaya ya Magharib B Unguja.

Amesema jamii inapswa kuelewa dhana ya ajira kuwa kuondokana na fikra ya kutaka kuajiriwa na serikali pekee na badala yake iamini katika shughuli zao wanazozifanya ambapo serikali imedhamiria kuwasaidia na kuzifanya ajira na shughuli walizonazo zinakuwa endelevu kwa ajili ya kujiingizia kipato na kujikwama katika janga la umasikini.

Kwa upande wake Kamishna wa Kazi Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Rashid Khamis Othman amesema kupitia kamati itakayoziduliwa hivi karibuni kuna matarajio makubwa ya kutatua changamoto za ajira kwa waajiri na waajiriwa ikiwemo suala la urasimu.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya zote za Unguja mkuu wa wilaya ya magharib B Bi Hamida Mussa Khamis amesema ikiwa kamati hizo zitaratibiwa kwa mujibu ya matarajio ya serikali chagamoto ya ajira iliyopo itaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka sambamba na kuahidi kuwa wilaya zipo tayari kusimamia mpango huo

Nae mshiriki wa kikao hicho ambae pia ni mjumbe wa kamati hiyo Othamn Mohd Abdallah (Makombora) amesema uwa vijana wanahitaji kufanyiwa haraka suala la utatuzi wa ukosefu wa ajira amewaomba kuwa wastahamilivu na kuingua mkono serikali katika kulitaftia ufumbuzi suala hilo.