Back to top

Spika Pelosi aizuru Taiwan licha ya vitisho.

03 August 2022
Share

Licha ya vitisho kutoka Beijing,nchini China Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, amewasili Taiwan na kuzungumza na Rais na Naibu Spika wa bunge, huku China ikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho.

Jeshi la China linafanya mazoezi ya kivita umbali wa kilomita 20 tu kutoka fukwe za Taiwan, likisema liko kwenye hali ya hadhari ya kiwango cha juu, tayari kuchukuwa hatua hatua yoyote kujibu uchokozi huo wa Marekani kama ikibidi.