Back to top

SUKARI ILIYOBAKI WILAYANI SONGEA NI CHINI YA TANI 10

04 February 2024
Share

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Bw.Wilman Ndile, amesema sukari wilayani humo imeadimika na kwamba akiba ya bidhaa hiyo iliyobaki kwenye Wilaya hiyo ipo chini ya tani 10, huku wafanyabiashara wakiuza bidhaa kwa bei ya kuanzia Tsh. 6000/= hadi Tsh. 7000/= kwa kilo moja.
.
Bw.Ndile amesema kutokana upungufu wa bidhaa hiyo, wamechukua hatua mbalimbali zikiwemo za kuruhusu malori kwenda nchi jirani ya Msumbiji kuchukua sukari, wakati taratibu zingine za vibali zikiendelea, ili kuhakikisha bidhaa hiyo inaendelea kupatikana.