Back to top

Suma JKT yatakiwa kuongeza kasi ujenzi shule ya Iyumbu.

14 September 2021
Share

Serikali imeliagiza shirika la Suma-JKT liongeze kasi ya ujenzi wa shule ya mfano Iyumbu ili ianze kutumika mwezi Januari mwaka 2022 kama ilivyokusudiwa.
.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omari Kipanga ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa chuo cha ufundi Nala na shule ya mfano Iyumbu miradi iliyo chini ya wizara hiyo.
.
Akiwa katika chuo cha ufundi Nala, amesema chuo hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi elfu tatu.
.
Akitoa taarifa ya ujenzi kwa Naibu Waziri, Naibu Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT Meja Geoffrey Ngole amesema ujenzi huo ulioanza Julai 2020, unatarajiwa kukamilika februari mwaka 2022.