Back to top

Taasisi za kifedha zibuni huduma nafuu - Majaliwa.

11 April 2022
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za fedha kubuni mbinu zitakazowezesha watanzania wengi kupata huduma rasmi za kibenki kwa gharama nafuu ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua na umasikini.
 
Mhe.Majaliwa ametoa wito huo katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya 'Teleza Kidijitali' inayotolewa na Benki ya NMB, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena jijini Dodoma.