
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Dk.John Mboya, amewataka viongozi, watumishi na wananchi mkoani humo, kuchangamkia fursa za uwekezaji katika Masoko ya Mitaji kwenye taasisi rasmi, zilizopewa dhamana na Serikali kufanya shughuli za uwekezaji kisheria ili kuweza kupata faida na kujikwamua kiuchumi.
Dkt.Mboya ametoa rai hiyo alipokutana na Timu ya wataalamu ya Wizara ya Fedha ambao wamefika mkoani humo kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali wakiwemo watumishi, wafanyabiashara na wajasiriamali.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha Wilaya ya Uyui, Bw.Cledus Mbawala, amesema kuwa katika ngazi ya Wilaya, Ofisi yake imekuwa ikifanya ufuatiliaji na kuhakikisha Taasisi zote zinazojihusisha na masuala ya fedha zinakuwa na leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania na zinafuata sheria na taratibu katika kutekeleza majukumu yao.
