Back to top

TADB yaombwa kuwawezesha wakulima wa ufuta mikopo yenye riba nafuu.

13 August 2020
Share

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Bw.Julius Mtatiro ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwainua wakulima wa ufuta wilayani humo kupitia mikopo yenye riba nafuu ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Bw.Mtatiro ametoa ombi hilo wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ofisini kwake Bw.Japhet Jastine na Kufafanua kuwa ikiwa wakulima watawezeshwa mapato ya ufuta yataongezeka kutoka bilioni tisa hadi.

Akijibu ombi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw.Justine amesema ataisaidia wilaya hiyo kuinua zao la ufuta.

Kwa upande wake mkulima mkubwa mkoani Ruvuma Bw.Isaya Mbilinyi ameiomba benki hiyo kufungua matawi zaidi wilayani na mikoani ambako wanalima mazao kwa wingi ili wakulima waweze kunufaika na benki yao.