Back to top

Tafiti zabaini vyanzo vikuu vitatu vya ajali.

24 May 2018
Share

Serikali imesema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na jeshi la polisi ajali za barabarani  husababishwa na vyanzo vikuu vitatu ambavyo ni vyanzo vya kibinadamu,kiufundi,na vya kimazingira.

Hayo yamesemwa bungeni na Mh Mwigulu Nchemba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati akijibu swali la Mh Emanuel Mwakasaka Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini aliyetaka kujua ajali za boda boda nyingi  zinasababishwa na askari polisi kukamata ovyo serikali ina mikakati gani kudhibiti hali hiyo.

Mh Nchemba akaongeza kuwa baadhi ya waendesha pikipiki wanauelewa mdogo kuhusu sheria za usalama  barabarani na mara nyingi pikipiki zao zina mapungufu jambo ambalo huwafanya kutojiamini.

Aidha akasema kuwa kutokana na na sababu hizo na nyingine nyingi waendeshaa boda boda wanapaswa kutambua na kutimiza wajibu wao katika kufuata sheria.

Mh Nchemba akaliambia bunge kuwa ili kuepukana na ajali za kizembe serikali kupitia jeshi la polisi itaendelea kutoa elimu kwa waendesha pikipiki ili kuwajengea uelewa wa sheria za usalama barabarani.