Back to top

TAKUKURU kamilisheni uchunguzi mapema-Majaliwa.

13 January 2020
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ukamilishe mapema uchunguzi dhidi ya madudu yaliyoibuliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 na wizi uliofanywa na viongozi wa AMCOS kwa wakulima wa ufuta na korosho ikiwemo wilaya ya Ruangwa.
 
Ameyasema hayo leo wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Ruangwa lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 142. Ametoa wito kwa TAKUKURU kuwa imara na kuweza kutembea kifua mbele katika mapambano hayo. 
 
Waziri Mkuu amesema  pamoja na TAKUKURU kuendelea na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku pia ameuagiza uongozi wa taasisi hiyo ukamilishe mapema utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa kwao kwa nyakati tofauti.