Back to top

TAKUKURU Ruvuma: Tunafanya uchunguzi wa ubadhirifu wa shilingi bil 3.

01 August 2021
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Ruvuma inafanyia uchunguzi upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 3 mkoani humo zinazodaiwa kuibiwa kwenye halmashauri kupitia mashine za kukusanyia pesa za posi.
.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Taasisi hiyo wa mkoa wa Ruvuma Bw. Hamza Mwenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha aprili hadi julai.
.
katika hatua nyingine Bw. Mwenda amewaonya matapeli wanaowatapeli watu kwa kuwapigia simu  hasa viongozi na kudai kuwa wao ni maofisa wa TAKUKURU kwamba  kuna mambo yao wanashughurikia na kuwaomba rushwa ili wasiwashughurikie.