Back to top

TAKUKURU yambana Muuguzi aliyeomba rushwa kwa mgonjwa

06 November 2019
Share

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU ) mkoani Tabora, imemfikisha mahakamani muuguzi mmoja wa hospitali ya wilaya ya Igunga kwa kosa la kuomba hongo ya shilingi laki mbili kutoka kwa mgonjwa wa kifua kikuu,kinyume cha sheria huku akiwa tayari alishapokea kiasi cha shilingi laki moja.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora kaimu kamanda wa TAKUKURU mkoani Tabora Bw.Mussa Chaulo amemtaja muuguzi mtuhumiwa wa kosa hilo, kwa jina la  Wellace Joseph Kaziri, ambapo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.