Back to top

TAKUKURU yatia mguu ubadhirifu milioni 142 Saccos manispaa ya Mtwara.

22 January 2021
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara imeanza kufuatilia tuhuma za ubadhilifu ya shilingi milioni 142 za chama cha akiba na mikopo (Saccos) Manispaa ya Mtwara/Mikindani zikiwemo fedha za watumishi waliostaafu na za watu waliokopeshwa bila kuwa wanachama wa chama hicho.

Hayo yamesemwa na mkuu wa TAKUKURU mkoani Mtwara Enock Ngailo wakati akiwakabidhi watumishi wastaafu jumla ya shilingi milioni 18 kati ya milioni 20 zilizookolewa kwenye operesheni kubwa za kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.

Kwa upande wao baadhi ya watumishi hao wastaafu, wameishukuru serikali kwa jitihada kubwa iliyofanya katika kuhakikisha malipo yao hayapotei.

Katika hatua nyingine TAKUKURU mkoani Mtwara imepokea malalamiko ya rushwa 149 katika kipindi cha miezi 3 cha oktoba hadi desemba mwaka jana 2020, huku halmashauri zikiongoza kuwa na malalamiko mengi.