Back to top

TAKUKURU:Vigogo wa idara ya afya mbaroni kwa kuomba na kupokea rushwa.

16 April 2021
Share

TAKUKURU mkoani Geita inawashikilia Afisa Afya Mazingira Kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili na Afisa Mazingira halmashauri ya mji wa Geita kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi laki moja kutoka kwa mmiliki wa kiwanda kidogo cha kubangua karanga ili wasimchukulie hatua kutokana na kiwanda hicho kuwa na mapungufu.
.
Akizungumza mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita Bw.Leonidas Felix amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Wambura Mkeha na Emanuel Michael ambao wote ni watumishi wa serikali.
.
TAKUKURU pia imewakamata maafisa watendaji thelathini wa vijiji wilayani Nyangwale kwa kugawana milioni thelathini na mbili walizozikusanya kupitia mashine za EFD kisha kuharibu mashine hizo.