Back to top

Taliban:wanawake marufuku kushiriki vipindi vya runinga

22 November 2021
Share

Wanawake wamepigwa marufuku kushiriki katika vipindi vya runinga nchini Afghanistan katika sheria mpya iliyowekwa na serikali ya Taliban.

Waandishi wa kike na watangazaji pia wametakiwa kuvalia hijabu katika runinga , ijapokuwa maelezo hayo mapya hayasemi wanafaa kujifunika kkwa namna gani.

Waandishi wa habari wanasema baadhi ya sheria hazieleweki na zinapaswa kutafsiriwa.