
Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mkoa wa Kinondoni Kusini, limewataka wafanyabiashara, wanaofanya biashara zao chini ya miundombinu ya TANESCO kwenye line kubwa ya msongo wa KV 220, kutoka mkoani Morogoro hadi mkoani Dar es Salaam, kuondoa biashara zao kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria.
.
Wito huo umetolewa na Afisa Usalama wa TANESCO, Mkoa wa KInondoni Kusini, Bi.Lilian William, katika oparesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao katika eneo la Mlandizi Sokoni, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
