Back to top

TANESCO YAAINISHA BEI ZA KUFUNGIWA UMEME.

29 January 2022
Share

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa mtwara limesema maeneo yote yenye huduma muhimu za kijamii gharama ya kuvuta umeme majumbani ni shilingi laki tatu na elfu ishirinini, huku maeneo yasiyo na huduma hizo yataendelea kulipa shilingi elfu ishirini na saba kama mambavyo sheria inaelekeza.

Kauli hiyo imetolewa na Mejena Tanesco mkoa wa Mtwara, Injinia Fadhili Chilombe wakati akitoa ufafanuzi wa bei za kuunganisha umeme majumbani kwenye kikao cha baraza la madiwani cha halmashauri ya mji Nanyamba wilaya ya Mtwara.

Amesema kwa hivi sasa hakuna tena umeme wa shilingi elfu ishirini na saba kwa wakazi wa mjini ama meneo yenye huduma zote za kijamiii ambao kwa sasa watalazimika kulipa shilingi laki tatu na elfu ishirini.

Kufuatia hilo amewataka madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi kuwaelimisha hilo ili kuondoa migogoro ambayo imenaweza kujitokeza baina ya Tanesco na wanchi.

Hata hivyo baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji Nanyamba wamesema pamoja na maboresho yanayofanywa katika shirika hilo ni vema nishati ya umeme ikawafikia wananchi wote ikiwa ni pamoja na maeneo yenye huduma muhimu za kijamii ikiwemo zahanati, vituo vya afya lakini pia kwenye miundombinu ya maji.


Mejena Tanesco mkoa wa Mtwara, Injinia Fadhili Chilombe amesema maeneo yote yenye huduma muhimu za kijamii gharama ya kuvuta umeme majumbani ni shilingi laki tatu na elfu ishirinini, huku maeneo yasiyo na huduma hizo yataendelea kulipa shilingi elfu ishirini na saba kama mambavyo sheria inaelekeza.