Rais Dakta. JOHN POMBE MAGUFULI amelitaka Shirika la Umeme Tanzania -TANESCO- liendelee kuchukua hatua zitakazofanya umeme kupatikana kwa bei nafuu kwa wananchi.
Rais amepongeza hatua ya kupunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wananchi nakutaka juhudi hizo ziendelee.
Rais MAGUFULI ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Mtambo wa Kufua Umeme wa Kinyerezi II Jijini Dar es Salaam.
Amesema umeme ni chachu ya maendeleo ya nchi, lakini umeme uliopo wa Megawati zaidi ya 1,500 bado hautoshi hivyo ametoa wito kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye kufua umeme kujitokeza kwamaslahi ya Watanzania na wawekezaji hao.