Back to top

TANESCO YAWASHA MTAMBO MPYA KINYEREZI ONE

17 June 2022
Share

Shirika la Umeme Tanesco limewasha mtambo mpya kati ya mitambo 4 inayotumia gesi asilia kutoka Songosongo, iliyojengwa Kinyerezi One ambapo Megawati 185 zitazalishwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande amesema hayo Dar es Salaam, nakueleza kuwa hatua hiyo itasaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa umeme wa uhakika hapa nchini.