Back to top

Tanesco yawatoa hofu wateja wao kuhusu njia ya kununua umeme.

31 March 2018
Share

Shirika la umemea nchini Tanzania Tanesco limewahakikishia wateja wake kuwa huduma za kununua umeme kwa njia ambazo walikuwa wanazitumia hapo awali zipo palepale na wasijaribu kununua umeme mwingi kwa haraka wakidhani kuwa kuanzia Aprili moja umeme hautapatikana kwani wakifanya hivyo watasababisha msongamano mkubwa usikokuwa na sababu.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Mhandisi Costa Rugagumya amewatoa hofu wateja wao kuwa hakutakuwa na shida yoyote na hivyo wanunue umeme kulingana na mahitaji yao.

Naye Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Tehama Bw. Demitruce Dashina amesema kilichotokea sasa kwa Tanesco siyo kipya bali ni jambo ambalo lilikuwa limepangwa na hata baadhi ya mashirika mengine ya umma yalishanza kuutumia mfumo huo Mpya.