Back to top

Tani Laki Moja na Elfu 30 za sukari kuzalishwa Kilombero.

23 May 2020
Share

Kiwanda cha Sukari cha Kilombero Mkoa ni Morogoro kimezindua utengenezaji wa sukari msimu huu matarajio yakiwa ni kutoa tani Laki Moja na Elfu 30 za sukari msimu huu.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa u tengenezaji sukari, Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kinachomilikiwa na Kampuni ya Ilovo, Balozi Ami Mpungwe amesema utengenezaji wa sukari katika kiwanda hicho umeongezeka kutoka tani Elfu Thelathini kwa msimu na kufukia tani laki moja na Elfu 30 kwa sasa baada ya uwekezaji mkubwa wa Shilingi zaidiya bilioni 240.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bwana Loata Ole Sanare alipozungumza baada ya kuzindua msimu mpya kiwandani hapo amekipongeza kiwanda hicho kwa kuanza u tengenezaji sukari wiki mbili kabla ya msimu.