Back to top

TANROADS mkoani Rukwa yatakiwa kuharakisha ujenzi wa kivuko mto Kale.

23 February 2021
Share

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Kituo Cha ITV juu ya daraja la Mto Kale linalounganisha vijiji 11 vya kata tatu za wilaya ya Kalambo kusombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara, hatimaye wajumbe wa Bodi ya Barabara mkoani Rukwa wameingilia kati suala hilo na kumwagiza Meneja wa TANROADS mkoani humo kuharakisha ujenzi wa kivuko cha muda kutokana na shughuli za usafirishaji kusimama huku ujenzi wake ukisuasua.


Hayo yamebainishwa kupitia kikao cha bodi ya barabara mkoani humo, ambapo wajumbe wa kikao hicho wamekiri kusikitishwa na kusuasua kwa ujenzi wa kivuko hicho.