
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Elimu, Sayansi, na Utamaduni(UNESCO) upande wa Tanzania Prof. Hamis Malebo amesema Tanzania iko hatarini kukosa wataalamu wa fani za Uhandisi, Sayansi na Teknolojia hali itakayopelekea kukwama kwa masuala mbalimbali ya kimaendeleo hasa wakati huu ambao nchi inapambana kuinua uchumi wa viwanda na ujenzi wa miundombinu.
