Back to top

TANZANIA IKO TAYARI KWA FAINALI ZA SOKA LA UFUKWENI BSAFCON 2024 MISRI

06 August 2024
Share

Kocha wa Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni, Jaruph Juma, amesema kwa maandilizi waliyofanya anaamini Timu hiyo itafanya vizuri kwenye Mashindano ya mwaka huu ya AFCON soka la Ufukweni, ambayo yamepangwa kufanyika kuanzia Oktoba 19–26, 2024, katika Jiji la kuvutia la Pwani ya Hurghada, Misri.

Jiji hilo linatarajiwa kuwakaribisha nchi ya Ghana, Senegal, Mauritania, Malawi, Morocco, Tanzania, Msumbiji, na wenyeji Misri, ambapo pia droo itafanywa ili kubaini jozi za hatua ya makundi ya shindano hilo.

Washindi kutoka katika shindano hilo, wataiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia la FIFA la Soka la Ufukweni, ambalo litaandaliwa nchini Ushelisheli mwaka ujao.