Back to top

Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Sweden.

17 January 2020
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Sweden katika Sekta ya Elimu, Uwekezaji wa Biashara, Utalii na Mazingira.

Makamu wa Rais ameyasema hayo Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg.

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano kati ya Nchi mbili hizi katika Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Uwekezaji wa kibiashara na Mazingira.

Nae Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe.Anders Sjoberg amemuahidi Makamu wa Rais kwamba Nchi yake itashirikiana Bega kwa Bega na Tanzania katika kuhakikisha kuwa Nchi mbili hizi zinafikia Malengo.