Back to top

Tanzania kuagiza chanjo za Corona zilizothibitishwa na WHO.

01 August 2021
Share

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata MulaMula amesema serikali itaendelea kuagiza aina mbalimbali za dawa za chanjo ya maambukizi ya virusi vya Corona zilizogunduliwa na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Amesema kabla ya kutoa chanzo hizo kwa wanachi, zitafanyiwa uchunguzi wa kina ili kuona kama hazina madhara kwa binadamu na kama zina uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi hayo.

Balozi MulaMula ametoa kauli hiyo mkoani Kagera alikoshiriki kwenye harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa vya Taasisi Mafunzo ya Afya ya Mtakatifu Magdalena, Wilayani Misenyi.

Amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti kuenea kwa maabukizi hayo pamoja  na mataifa mengine.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali William Sakulo amesema wilaya hiyo hadi jana ilikuwa na wagonjwa 19 waliolazwa kwenye vituo vya afya.