Back to top

Tanzania kunufaika, fedha za Kukuza Uwekezaji

29 September 2022
Share

Mwenyekiti wa timu ya Afrika ya KEIZAI DOYUKAI (Japan Association of Corporate Executives), Bw. Mutsuo Iwai amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zitakazonufaika na fedha za Mfuko wa Kukuza Uwekezaji barani Afrika kutoka Serikali ya Japan zitakazotolewa kuanzia Machi, 2023.
.
Bw.Iwai ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa ofisini kwao Marunouchi, Chiyoda-ku, jijini Tokyo, Japan, ambapo amebainisha kuwa fedha hizo za uwekezaji kwenye mitaji (start-ups) zimelenga kukuza biashara ambazo zitatatua changamoto za kijamii zikiwemo sekta za afya, kilimo, nishati na kuimarisha uhifadhi wa mazingira.