Back to top

TANZANIA KUOMBA KUWA MWENYEJI AFCON 2027

24 May 2023
Share

Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda kupitia Pamoja Bid wamedhamiria kuwa mwenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (African Cup of Nations) 2027.
.
Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo amebainisha kuwa nchi hizo zinawania nafasi hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Michezo imepata, hivyo kuwa wenyeji wa AFCON 2027 kutaongeza hamasa zaidi kwa ukuaji wa michezo hususan soka.