Back to top

Tanzania kuwekeza kwenye matumizi ya filamu kutangaza utalii

22 February 2020
Share

Wizara ya maliasili na utalii  kwa kushirikiana na bodi ya filamu nchini imeandaa mkakati wa kutumia mfumo wa filamu kutangaza vivutio vilivyopo nchini zikiwemo hifadhi za taifa  ili  kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini.

Utekelezaji wa mkakati huo kwa mujibu wa katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Profesa Adolph Mkenda utayashirikisha makampuni makubwa ya filamu kutoka nje na kwamba nguvu kubwa itaelekezwa kwenye utangazaji wa hifadhi ambazo bado hazijatambulika zaidi kimataifa.

Ili kufanikisha mpango huo kaimu katibu  mtendaji wa bodi ya filamu nchini Dkt.Kiagho Kilonzo anasema wameanza kuondoa urasimu wa upatikanaji wa vibali vya waandaaji wa filamu  kuingia nchini
Mpango huo pia unawashirikisha wadau wengine wa sekta ya utalii nchini ambao wameahidi kuwekeza nguvu kuufanikisha.