Back to top

TANZANIA NA IVORY COAST KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA MICHEZO

26 January 2024
Share

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ameipongeza Ivory Coast, kwa maandalizi mazuri ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), yanayoendelea kufanyika kwenye nchi hiyo ambapo amebainisha kuwa Tanzania inajifunza mengi kupitia nchi hiyo, kwa kuwa itakua mwenyeji wa michuano hiyo kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.
.
Mhe.Ndumbaro ameyasema hayo, leo Januari 26, 2024, alipokutana na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast, Mhe. Adjé Silas, ambapo katika mazungumzo yao wamejadili juu ya kusaini Makubaliano Maalum ya Ushirikiano (MOU), katika sekta ya michezo baina ya nchi hizo ili kuibua na kukuza vipaji.