
Maafisa wa serikali za Tanzania na Kenya,wameanza zoezi la kuhakiki mipaka na kurudishia upya alama za kutengenisha nchi hizo mbili za Afrika Mashauri,ikiwa ni sehemu za utekelezaji wa azimio la umoja wa nchi za Afrika linalotaka nchi wanachama kuhakikisha,kuimarisha na kuboresha mipaka yake iliyowekwa na wakoloni ili kuepusha nchi hizo kuingia katika migogoro.
Katika zoezi hilo ambalo limeanza rasmi Machi 28 mwaka huu upande wa mkoa wa Mara baada ya maafisa hao wa idara mbalimbali za serikali za nchi hizo mbili kushiriki katika mafunzo maalum ya kusimamia zoezi hilo,litahusisha mpaka wa Kenya na Tanzania wenye urefu wa kilometa 760,hatua ambayo inalenga kukabiliana pia na ongezeko la watu katika nchi hizo mbili.
Kwa upande wake mwakilishi wa nchi ya Kenya Bw. George Natembea,amesema hakuna kasoro kubwa kwa mpaka wa Tanzania na Kenya,lakini amesema ni jambo la busara ambalo limefanywa na viongozi wa serikali hizi mbili kufanya maboresho hayo hivi sasa ili kuondoa kasoro zinazoweza kujitokeza kati ya nchi na nchi.