Back to top

TANZANIA NA ZAMBIA KUONDOA VIKWAZO VYA KIBIASHARA

02 August 2022
Share

Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia, Mhe.Hakainde Hichilema ambaye alikuwa nchini kwa ziara ya siku moja wamekubaliana mambo kadhaa ikiwemo kurudisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili pamoja na kuondoa vikwanzo vya biashara, ambavyo wafanyabiasahrea wa pande zote wanakumbana nazo.

Akizungumza Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kuwa na mazungumzo na mgeni wake huyo, Mhe.Samia wamekubaliana kurudisha uhusiano ambao kwa muda mrefu umepotea.

Kwa upande wake Mhe.Hichilema amepongeza jitihada mbalimali zinazofanywa na Serialki ya Tanzania ikiwemo, Wizara ya Madini kwa namna ambayo wameweza  kuwasimamia wachimbaji wadogo wadogo pamoja na kurasimisha biashara ya madini.