Back to top

Tanzania inaadhimisha Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika jijini Mwanza.

09 December 2019
Share


Taifa leo lina adhimisha miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika na baadhi ya viongozi wa Dini Mkoani Mtwara wamewataka Watanzania kuenzi amani iliyoasisisiwa na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kuleta ustawi wa nchi.

Viongozi hao wa dini wamesema hayo kwenye ibada iliyotumika pia kuliombea taifa.

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Mtwara, Sheikh Nurdin Mangochi ametaka uhuru usiishie kwa kufurahia taifa kupata uhuru, bali uambatane na Watanzania wenyewe kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuimarishwa kwa huduma za jamii.

Leo ni mapumziko, uongozi wa ITV/Radio One utawatakia mapumziko mema ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika.