Back to top

TANZANIA YAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI BASEBALL 5

23 May 2022
Share

Timu ya taifa ya Baseball 5 imefuzu hatua ya robo fainali kwenye michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia baada ya ushindi katika michezo yake miwili ya kundi B leo.

Tanzania imeshinda kwa seti 2-0 dhidi ya Zambia katika mchezo wa kwanza kwa kuibuka na ushindi wa pointI 14 kwa 2 seti ya kwanza na pointi 4-1 seti ya pili, huku pia ikishinda kwa seti 2-1 dhidi ya Burkina Faso kwa kuibuka na ushidi wa pointi 1-3 6-3 na 15-6.

Tanzania kesho itacheza na Kenya saa 7:30 mchana ikiwania kumaliza kinara wa kundi B.

Awali leo Tanzania ilikuwa ianze na Misri lakini kwakuwa Misri hawajaleta timu Tanzania sasa inapata ushindi wa mezani na kuwa na ushindi wa mechi 3 mfululizo.