Back to top

TANZANIA YAIPATA MIKOPO YA DOLA BIL.1 KUTOKA KOREA KUSINI

15 September 2023
Share

Serikali ya Jamhuri ya Korea imeiwezesha Tanzania kupata mikopo yenye masharti nafuu kutoka Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi wa Korea, yenye thamani ya  Dola za Marekani bilioni moja, kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.

Taarifa ya Wizara ya Fedha imesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum, amesema hayo katika mazungumzo yake na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi na Fedha wa Korea, Kyungho Choo, mjini Busan, Korea Kusini.

Amesema mikopo hiyo imesaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali katika pande zote mbili za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadhi ya miradi iliyoidhinishiwa fedha mwezi Februari, 2023 ipo katika hatua mbalimbali za maandalizi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi na Fedha wa Korea KYUNGHO CHOO, amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.